Katiba ya Kenya

(Elekezwa kutoka Katiba ya mwaka 2010)

Katiba ya Kenya ndiyo sheria kuu kabisa ya Jamhuri ya Kenya. Katiba ya mwaka 2010 ilichukua nafasi ya katiba ya wakati wa uhuru ya mwaka 1963.

Katiba hiyo alipatiwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya tarehe 7 Aprili 2010, ikachapishwa rasmi tarehe 6 Mei 2010 na kuwekewa kura ya maoni tarehe 4 Agosti 2010[1].

Ilipitishwa kwa kura 67%[2] na kutangazwa tarehe 27 Agosti 2010[3].

Historia

Katiba ya mwaka 1963, ilirekebishwa katika mwaka 1969. Marekebisho yalibadilisha Kenya kutoka mfumo wa shirikisho, uliokuwa ukijulikana kama mfumo wa majimbo, hadi mfumo wa umoja na kuifanya bunge iwe ya chumba kimoja. Serikali ilibadilika kutoka mfumo wa kibunge hadi mfumo wastani wa kirais, ikiwa na rais mwenye nguvu zaidi. Ulinzi wa orodha ya haki ulipunguzwa. Marekebisho mengine yalifanyika mwaka 1982. Yaliifanya Kenya kuwa nchi ya chama kimoja.[4]

Madai ya kuwa na katiba mpya yalianzia miaka ya 1990. Mfumo wa chama kimoja ulibadilishwa tena mwaka 1991, na uchaguzi wa kwanza wa urais ukafanyika mwaka 1992. Mwaka 2002, chama cha Muungano wa Mpinde wa Kitaifa (NARC) kilishinda uchaguzi. Mashauriano baina ya serikali na mashirika ya kiraia yalifanya kuwepo kwa "Katiba Rasimu ya Bomas".[4] Ilipigiwa kura ya maoni tarehe 21 Novemba 2005 lakini haikupitishwa.

Rasimu ya katiba ya 2010 iliandikwa na Kamati ya Wataalamu na kuchapishwa kwa umma tarehe 17 Novemba 2009 ili kuwezesha mjadala wa umma na bunge iamue kama ingetaka ipigiwe kura ya maoni. Umma ulipatiwa muda wa mwezi mmoja kuikagua na kupeleka mapendekezo na marekebisho kwa wabunge wao. Rasimu rekebishe ilipelekwa kwa Kamati ya Bunge ikarekebishwa na kurudishwa kwa Kamati ya Wataalamu. Waliichapisha Katiba Iliyopendekezwa tarehe 23 Februari 2010, iliyopelekwa bungeni ipigwe msasa.[5]

Bunge Ilipitisha katiba hiyo kwa pamoja tarehe 1 Aprili 2010. Ilipelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya tarehe 7 Aprili 2010, ikachapishwa rasmi tarehe 6 Mei 2010 na kufanyiwa kura ya maoni tarehe 4 Agosti 2010. Ilipitishwa na wapigakura 67%.

Faida zilizopatikana

  • Orodha ya Haki inayotambua haki za kijamii na kiuchumi za wananchi (Sura ya Nne)
  • Kutolewa kwa kikomo cha miaka 35 kwenda chini kwenye ofisi ya rais. (Kipengee cha 137(b))
  • Haki ya kutolewa kwa wabunge na maseneta na wananchi. (Kipengee cha 104)
  • Uwakilishaji katika mashirika na vyombo vya kiserikali lazima uzingatie kutokuwepo na jinsia inayozidi thuluthi mbili katika mtungo wake. (Sura ya 7, Kipengee cha 81(b))
  • Sura ya Maadili, inahitaji kuwepo kwa Tume Huru ya Maadili, iangalie kuzingatiwa kwa maadili katika taasisi zote za kiserikali. (Sura ya sita)
  • Tume ya Usawa na Haki za Binadamu iliyo na nguvu za kuwaita na kuwachunguza watu waliohusika katika ukiukaji wa haki za binadamu katika serikali na umma. (Kipengee cha 252)
  • Ugavi wa usawa wa mali kati ya serikali ya kitaifa na kaunti kupitia bunge. (Sura ya 12, Sehemu ya 4)
  • Hazina ya Usawa ili kuboresha mahitaji ya jamii zilizotengwa. (Kipengo cha 204)
  • Mtu yeyote kutoka umma anaweza kushtaki serikali kwa kukiuka Haki za Binadamu na Orodha ya Haki. (Kipengee cha 23 (1)(2))
  • Tume ya Mishahara na Malipo ina nguvu za kupitia mishahara ya maafisa wote wa serikali na kuhakikisha kuwa bili ya malipo inaweza kumudiwa. (Kipengee cha 230(5))
  • Uhuru wa mahakama umehakikishwa. (Kipengee cha 160)
  • Tume ya Kitaifa ya Ardhi ilitengenezwa kuchunga na kusimamia ardhi yote ya umma na ya serikali ya kitaifa na kaunti, kupendekeza sera za kushughulikia malalamiko kutoka umma, kushauri serikali ya kitaifa jinsi ya kuboresha usimamizi wa ardhi za kitaifa na kaunti, upangaji na kutatua migogoro. (Kipengee cha 167)
  • Haki za Mazingira zimetambuliwa. (Sura ya 5, Sehemu 2)
  • Uhuru wa vyombo vya habari.

Muundo wa serikali

Kilicho kipya katika katiba hii ni:

Serikali

Utendaji

Katika kilele cha utendaji, kuna rais, naibu wa rais na baraza la mawaziri

Bunge

Chumba cha juu - Seneti
  • Kila moja ya kaunti 47 ina seneta
  • Seneta huchaguliwa na wapiga kura
  • Jumla ya maseneta ni 60
  • Itasimamia mashtaka ya kuondolewa kwa rais (kipengee cha 145)
Chumba cha chini - Bunge la Taifa
  • Kuna maeneo bunge 290
  • Kila eneo bunge litachagua mjumbe
  • Kuna Wanawake Wajumbe 47 kutoka kaunti
  • Litachagua kumchunguza na kupitisha mashtaka ya kuondolewa kwa rais
Mabunge ya Kaunti na utendaji wake
  • Nchi imegawanywa kati ya kaunti 47
  • Kila kaunti ina Kamati ya Utendaji inayoongozwa na Gavana.
  • Bunge la Kaunti lina wajumbe waliochaguliwa kutoka Wadi

Mahakama

Kuna mahakama kuu tatu:

  • Mahakama ya Upeo - Korti la juu kabisa linalotungwa kwa Jaji Mkuu, Naibu wa Jaji Mkuu na majaji wengine watano. Linashughuliki rufaa kutoka Korti la Rufaa na Korti la Katiba. Pia, litasimamia mashtaka ya kuondolewa kwa rais.
  • Mahakama ya Rufaa - hushughulikia kesi za rufaa kutoka Mahakama Kuu. Ina majaji ambao hawapungui 12 na huongozwa na rais anayeteuliwa na jaji mkuu.
  • Mahakama Kuu

Kuna Tume Huduma ya Mahakama, iliyo huru, inayoshughulikia uteuzi wa majaji

Mwanasheria Mkuu

  • Huteuliwa na rais na kuidhinishwa na Bunge la Taifa
  • Hushikilia hatamu kwa muhula mmoja wa miaka sita pekee

Tazama pia

Marejeo

Soma zaidi