Ladislaus I wa Hungaria

Ladislaus I wa Hungaria (kwa Kihungaria: László; kwa Kiserbokroatia na Kislovakia: Ladislav I; kwa Kipolandi: Władysław; kwa Kilatini Ladislaus; Krakow, Polandi, 1040 hivi – Nitra, Slovakia, 29 Julai 1095) alikuwa mfalme wa Hungaria (kuanzia mwaka 1077) na wa Kroatia (kuanzia mwaka 1091) hadi kifo chake.

Mt. Ladislaus katika Chronica Hungarorum

Mtoto wa pili wa Béla I, alijitahidi kurudisha hali ya usalama nchini kwa kutunga sheria kali. Kwa kuteka Kroatia karibu yote, alianza upanuzi wa Hungaria na kwa kushinda Wapekenegi na Wakumani alihakikisha mipaka ya mashariki kwa miaka 150 iliyofuata.

Wakati wa utawala wake alirekebisha pia maadili na hali ya kiroho ya nchi kama vilivyokuwa chini ya Stefano wa Hungaria, na kueneza imani ya Kikristo nchini Kroatia, akianzisha jimbo la Zagreb.

Mwenyewe aliishi kwa sala na toba[1].

Alifariki vitani akipigana na Bohemia akazikwa Oradea, leo nchini Romania.

Papa Celestino III alimtangaza mtakatifu tarehe 27 Juni 1192. Hata binti yake, Irene wa Hungaria, malkia wa Dola la Roma Mashariki, anaheshimiwa vile.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Juni[2].

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

Vikuu

Vingine

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.