Kassim Majaliwa

(Elekezwa kutoka Majaliwa Kassim Majaliwa)

Kassim Majaliwa (alizaliwa 22 Disemba 1960) ni mwanasiasa nchini Tanzania na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kassim Majaliwa


Waziri Mkuu wa Tanzania
Aliingia ofisini 
19 Novemba 2015

tarehe ya kuzaliwa22 Desemba 1960 (1960-12-22) (umri 63)
Ruangwa
utaifaMtanzania
chamaChama Cha Mapinduzi
mhitimu wachuo cha ualimu Mtwara
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Chuo Kikuu cha Stockholm
taalumamwanasiasa nchini Tanzania
Fani yakeMwalimu

Maisha

Majaliwa ni mwenyeji wa Mnacho katika Wilaya ya Ruangwa aliposoma shule ya msingi kati ya mwaka 1970 hadi 1976. Akaendelea kusoma kwenye Shule ya Sekondari Kigonsera hadi 1980.

Miaka 1984-1986 alifanya kazi ya ualimu huko Lindi na tangu 1988 aliajiriwa na wizara ya elimu. Mwaka 1991 akajiunga na chuo cha ualimu Mtwara akaendelea na masomo ya digrii ya kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, masomo ya digrii ya pili kwenye Chuo Kikuu cha Stockholm (Uswidi) aliyomaliza 1999.

Mwaka 2000 alipewa kazi ya Mkuu wa Wilaya.

Alikuwa kwanza mbunge wa jimbo la Ruangwa tangu mwaka 2010 akigombea kwa CCM.

Aliwahi kushika vyeo vya naibu waziri wa utawala wa mikoa na serikali ya mitaa katika ofisi ya waziri mkuu tangu mwaka 2010[1] [2]na mkuu wa mkoa wa Lindi kuanzia 2006 hadi 2010.

Tarehe 19 Novemba 2015 aliteuliwa na rais John Magufuli kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania.[3]

Ni mpenzi wa michezo ya klabu za Tanzania na ni shabiki wa Simba S.C..

Marejeo

Viungo vya nje

Ofisi za Kisiasa
Alitanguliwa na
Mizengo Kayanza Peter Pinda
Waziri Mkuu wa Tanzania
2015-
Akafuatiwa na
[[]]