Mlinganyo
Mlinganyo (kutoka kitenzi "kulinga") katika hisabati (aljebra) ni kauli inayosema kuwa viwango viwili ni sawa yaani vinalingana. Milinganyo yote hutumia alama ya "="
kama vile 2 + 3 = 5
ambayo inasema "mbili ongeza tatu inalingana na tano".
Mlinganyo wa undani zaidi unatumia alama kwa viwango visivyojulikana awali na vinapaswa kugunduliwa,
Mfano :
3x + 3 = 9
Suluhisho linapatikana kwa kufuata hatua zinaopeleka "x" peke yake upande mmoja wa mlinganyo. Hatua hizi zinapaswa kuwa sawa pande zote mbili:
- 3x + 3 - 3 = 9 -3 (ondoa 3 pande zote mbili)
- 3x = 6
- 3x : 3 = 6 : 3 (gawanya kwa 3 pande zote mbili)
- x = 2
Hapo kazi ni kujua maana ya x ni nini ambayo ni 2 katika mfano huu.
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mlinganyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoFasihi simuliziAina za manenoShairiVivumishiMikoa ya TanzaniaOrodha ya makabila ya TanzaniaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaLughaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoKamusi za KiswahiliMofimuFasihiNembo ya TanzaniaMawasilianoSentensiMarie AntoinetteKamusiMange KimambiKumaViwakilishiAlama ya uakifishajiKitenziFani (fasihi)TamthiliaVitendawiliNominoKiswahiliMaudhuiSilabiTanzaniaJumuiya ya Afrika MasharikiKisaweVieleziYoung Africans S.C.Kiwakilishi nafsiDiamond Platnumz