Nicole Scherzinger

Nicole Prescovia Elikolani Valiente Scherzinger[1] (pia anajulikana kama Nicole Kea) (amezaliwa tar. 29 Juni 1978) ni mwimbaji wa R&B, mtunzi wa nyimbo, mnenguaji, mwanamitindo, na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa kuwa kama mwimbaji kiongozi wa kundi la muziki la The Pussycat Dolls. Amechekua jina la Scherzinger kwa sababu alilielewa na baba wa kufikia aliyekuwa Mjerumani.

Nicole Scherzinger
Nicole mnamo Agosti 2012
Nicole mnamo Agosti 2012
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwaNicole Elikolani Prescovia Valiente
Pia anajulikana kamaNicole Kea
Amezaliwa29 Juni 1978 (1978-06-29) (umri 45)
Honolulu, Hawaii, Marekani
Asili yakeR&B, hip hop, pop
Kazi yakeMwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mnenguaji, mwigizaji, mwanamitindo
Miaka ya kazi2001–hadi leo
StudioPolydor, A&M, Interscope
Ame/Wameshirikiana naPussycat Dolls, Days of the New, Timbaland, Sean Combs, Keri Hilson, T.I., Will.I.Am, Sean Garrett, Will Smith, Nelly, Rihanna
Tovutiwww.hernameisnicole.com

Wasifu

Maisha ya awali

Scherzinger alizaliwa mjini Honolulu, Hawaii na baba Mfilipino na mama Mhawaii/Mrusi.[2] Mama yake aliitwa Rosemary, na wakati ana mzaa Scherzinger alikuwa na umri wa miaka kumi na minane na wakawa wanaishi mjini inner city, lakini baadaye familia ikatengana wakati Scherzinger bado mdogo.

Baadaye familia ikaamia rasmi mjini Louisville, Kentucky wakati huo alikuwa na umri wa miaka sita, akiwa pamoja na ndugu yake wa kike aitwaye Ke'ala aliyezaliwa na baba Mjerumani Mwamerika Bw. Gary Scherzinger.[3][4]

Maisha binafsi

Kwa sasa Scherzinger anatembea na Lewis Hamilton, kukiwa na fununu za kusema kuwa wawili hao wataoana punde.

Muziki

Makala kuu ya: Albamu na Nyimbo za Nicole Scherzinger
Tazama pia Eden's Crush na Albamu na Nyimbo za Pussycat Dolls kwa taarifa ya albamu na kazi alizofanya akiwa pamoja na hilo kundi.

Albamu

  • 2009: Her Name Is Nicole

Single

  • 2007: "Whatever U Like" akimshirikisha T.I.
  • 2007: "Baby Love" akimshirikisha will.i.am
  • 2007: "Supervillain" akimshirikisha Mad Scientist (Digital Release Only)
  • 2007: "Puakenikeni" akishirikiana na Brick na Lace (Toleo la Mtandaoni Tu)
  • 2008: "Rio" (Caress Brazilian Mix) (Toleo la Mtandaoni Tu)

Single alizoshirikishwa

  • 2006: "Lie About Us" (Avant akimshirikisha Nicole Scherzinger)
  • 2006: "Come to Me" (Diddy akimshirikisha Nicole Scherzinger)
  • 2007: "You Are My Miracle" (Vittorio akimshirikisha Nicole Scherzinger)
  • 2008: "Scream" (Timbaland akimshirikisha Keri Hilson na Nicole Scherzinger)

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: