Will Smith

Willard Christopher "Will" Smith, Jr. (amezaliwa tar. 25 Septemba 1968)[1] ni mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, na rapa kutoka nchini Marekani. Amefurahia sana mafanikio yake ya kimuziki, televisheni na filamu. Gazeti la "Newsweek" limemwita mwigizaji mwenye uwezo mkubwa kabisa duniani.[2] Smith amewahi kushindanishwa kwenye tuzo za Golden Globe mara nne, Academy Awards mara mbili, na ameshinda matuzo kede-kede ya Grammys.

Will Smith

Will Smith mnamo 2019
AmezaliwaWillard Christopher Smith, Jr.
25 Septemba 1968 (1968-09-25) (umri 55)
Wynnefield, Philadelphia, Pennsylvania, West Philadelphia, Pennsylvania, U.S.
Kazi yakeMwigizaji, rapa, mtayarishaji wa filamu, mtayarishaji wa rekodi, mtayarishaji wa televisheni
Miaka ya kazi1987–hadi leo
NdoaSheree Zampino (1992–1995)
Jada Pinkett Smith (1997–hadi leo)
Tovuti rasmi

Smith ameanza kujibebea umaarufu akiwa kama rapa chini ya jina la The Fresh Prince mwishoni mwa miaka ua 1980 na jina la uhusika kwenye mfululizo wa televisheni wa The Fresh Prince of Bel-Air. Filamu maarufu ambazo kacheza ni pamoja na Bad Boys na mfululizo wake wa pili Bad Boys II; Men in Black na mfululizo wake wa pili Men in Black II; Independence Day; I, Robot ; Ali; The Pursuit of Happyness; I Am Legend; Hancock; na Seven Pounds. Yeye ni mwigizaji pekee katika historia kuwa na mfululizo wa filamu nane zilizopata mauzo ya dola za Kimarekani milioni 100 kwenye sanduku la ofisi la nyumbani na vilevile kuwa kama mwigizaji pekee kuwa na filamu nane mfululizo kushika nafasi ya kwanza kwenye siku ya uzinduzi wa nyumbani akiwa kama mwigizaji kiongozi.[3]

Familia na maisha ya mwanzoni

Smith, ni Mwafrika-Mwamerika aliyezaliwa na kukulia mjini West Philadelphia na Germantown huko Northwest Philadelphia. Mama yake, Caroline, alikuwa msimamizi wa shule ambaye alifanya kazi kama msimamizi wa bodi ya shule Philadelphia, na baba yake, Willard Christopher Smith, Sr., alikuwa mhandisi wa majokofu.[4][5] Kiimani, alilelewa Kibaptist.[6] Wazazi wake walitengana akiwa na umri wa miaka kumi na tatu na kuja kupeana talaka rasmi akiwa na umri wa miaka thelathini na mbili.[7] Ucheshi wa Smiths na jinsi anavyoonekana akiwa shuleni, wakampa jina la utani kama "Prince", ambalo hatumaye likaja kugeuka na kuwa "Fresh Prince". Wakati yuujanani mwake, Smith akaanza kurao na hatimaye akaanza kushirikiana na Jeff Townes (a.k.a. DJ Jazzy Jeff), ambaye alikutana naye kwenye sherehe moja hivi. Akanza kuhudhuria kwenye shule ya Overbrook High School ya mjini West Philadelphia. DJ Jazzy Jeff & The Fresh Prince ilizaliwa na Smith huku yeye akiimba mistari wakati Townes anashughurikia suala zima la kusugua na kuchanganya midundo—mwungano huo ulikuwa gumzo sana kwenye nyanja za muziki wa hip hop hasa katika miaka ya 1980 na mwazoni mwa 1990.

Diskografia

Makala kuu ya: Diskografia ya Will Smith
  • Big Willie Style (1997)
  • Willennium (1999)
  • Born to Reign (2002)
  • Lost and Found (2005)

Filmografia

MwakaFilamuUhusikaMshahara (US$)[8]Maelezo
1990Saturday Morning VideosHostTV
ABC Afterschool Special - "The Perfect Date"HawkerTV
The Fresh Prince of Bel-AirWilliam "Will" SmithTV (1990-1996)
1992BlossomFresh PrinceTV, Kauza sura
Where the Day Takes YouManny50,000
1993Made in AmericaTea Cake Walters100,000
Six Degrees of SeparationPaul500,000
1995Bad BoysDetective Mike Lowrey2,000,000
1996Independence DayCaptain Steven "Steve" Hiller, USMC5,000,000
1997Men in BlackJames Darrell Edwards / Agent J5,000,000
1998Enemy of the StateRobert Clayton Dean14,000,000Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
1999Torrance RisesKauza sura
Wild Wild WestCaptain James "Jim" West7,000,000
2000Welcome to HollywoodYeye mwenyewe
The Legend of Bagger VanceBagger Vance10,000,000Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
2001AliMuhammad Ali20,000,000Kashindanishwa — Academy Award for Best Actor
Kashindanishwa — Broadcast Film Critics Association Award for Best Actor
Kashindanishwa — Golden Globe Award for Best Actor – Motion Picture Drama
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
2002Men in Black IIJames Darrell Edwards / Agent J20,000,000
+ 10% ya mapato ya filamu
BET Award for Best Actor
Kashindanishwa — Black Reel Awards of 2002
Girlfriend ya B2KYeyey mwenyeweMuziki wa video
2003Bad Boys IIDetective Mike Lowrey20,000,000
+ 20% ya mapato yote ya filamu
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
2004A Closer WalkMwadithiajiMakala
Jersey GirlYeye mwenyeweKauza sura tu
American ChopperYeye mwenyeweTV, Kauza sura
I, RobotDetective Del Spooner28,000,000Mtayarishaji
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
Shark TaleOscar15,000,000Sauti
2005There's a God on the MicMakala
HitchAlex "Hitch" Hitchens20,000,000BET Award for Best Actor
Kashindanishwa — Black Movie Award for Best Actor
Kashindanishwa — Black Reel Awards of 2006
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
2006The Pursuit of HappynessChris Gardner10,000,000
+ 20% of the gross
Mtayarishaji

Kashindanishwa— Academy Award for Best Actor
Kashindanishwa — Black Reel Awards of 2007
Kashindanishwa — Broadcast Film Critics Association Award for Best Actor
Kashindanishwa — Chicago Film Critics Association Award for Best Actor
Kashindanishwa — Golden Globe Award for Best Actor – Motion Picture Drama
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
Kashindanishwa — Screen Actors Guild Award for Outstanding Performance by a Male Actor in a Leading Role

2007I Am LegendDr. Robert Neville25,000,000Mtayarishaji, Kashindanishwa — BET Award for Best Actor
Kashindenishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
2008HancockJohn Hancock20,000,000
+ 20% ya mapato ya filamu
Mtayarishaji
Lakeview TerraceMtayarishaji
The Secret Life of BeesMtayarishaji
Seven PoundsTim ThomasMtayarishaji
2009The Mark[9]
Unbroke: What You Need to Know About MoneyTelevision special
2010Time Share[10]
2011I Am Legend: Awakening[11][12]Robert Neville
2012Men in Black III[13]James Darrell Edwards / Agent J

Soma zaidi

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Will Smith kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.