Nona

Nona wa Nazianzo (305 hivi - 374 hivi) alikuwa mke wa Gregori Mzee na mama wa Gregori wa Nazianzo, Sesari wa Nazianzo na Gorgonia wa Nazienzi. Aliishi huko Kapadokia, mkoa wa Dola la Roma katikati ya Uturuki wa leo.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu pamoja na familia yake yote.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Agosti[1].

Maisha

Baada ya kuolewa , Nona alimsaidia Gregori mumewe kuongokea Ukristo kutoka madhehebu yenye mchanganyiko wa Uyahudi na Upagani yaliyomuabudu Hypsistos, Mungu "Aliye Juu".

Aliishi mpaka baada ya kifo cha mumewe, aliyefikia uaskofu, na ya wanae wawili.[2]

Mwanae maarufu zaidi, Gregori, ambaye pia alifikia uaskofu na anaheshimiwa kama mwalimu wa Kanisa, alitangaza sifa za mamaye[3]

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.