Nusutufe ya kusini
Nusutufe ya kusini (pia nusudunia ya kusini; Kiing.: Southern Hemisphere) ni nusu ya Dunia ilioko upande wa kusini wa ikweta.
Tofauti na nusutufe ya kaskazini hii ya kusini ina maeneo makubwa zaidi ya bahari ambayo ni asilimia 80.9, ilhali kaskazini ni asilimia 60.7 pekee. Theluthi moja tu, yaani 32.7%, za nchi kavu ya Dunia iko kwenye nusutufe ya kusini.[1]
Kati ya mabara ni Antaktiki na Australia nzima, asilimia 90 za Amerika Kusini na theluthi ya kusini ya Afrika yaliyopo kwenye nusutufe hiyo. Kuna pia visiwa vikubwa vya Asia kusini kwa ikweta na visiwa vingi vya Pasifiki. [2]
Majira ya joto ni kuanzia Disemba hadi Machi, na majira ya baridi kuanzia Juni hadi Septemba.
Tazama pia
- Nusutufe ya kaskazini
- Ikweta
- Tropiki ya Saratani
- Tropiki ya Kaprikoni
- Duara la Aktiki
- Duara la Antaktika
Marejeo
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoFasihi simuliziAina za manenoShairiVivumishiMikoa ya TanzaniaOrodha ya makabila ya TanzaniaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaLughaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoKamusi za KiswahiliMofimuFasihiNembo ya TanzaniaMawasilianoSentensiMarie AntoinetteKamusiMange KimambiKumaViwakilishiAlama ya uakifishajiKitenziFani (fasihi)TamthiliaVitendawiliNominoKiswahiliMaudhuiSilabiTanzaniaJumuiya ya Afrika MasharikiKisaweVieleziYoung Africans S.C.Kiwakilishi nafsiDiamond Platnumz