Papa Celestino V

Papa Celestino V, O.S.B. (121519 Mei 1296) alikuwa Papa kuanzia tarehe 5 Julai/29 Agosti 1294 hadi 13 Desemba 1294[1]. Alitokea Molise, Italia[2].

Mt. Selestini V.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Pietro Angelerio wa Morrone. Baada yake hakuna tena Papa aliyejichagulia jina la Celestino.

Alimfuata Papa Nikolasi IV baada ya miaka miwili ya pengo[3], akichaguliwa kutokana na umri wake mkubwa na sifa ya utakatifu na utendaji miujiza.

Ni maarufu kwa kuwa mwaka uleule alijiuzulu[4] kwa kujitambua hawezi Upapa [5] ili arudi kuishi maisha ya upwekeni kama mmonaki (mwaka 1244 alikuwa ameanzisha shirika la Waselestini, tawi la Wabenedikto)[6]. Lakini Papa Bonifasi VIII aliyemfuata alimfunga akafuta karibu maamuzi yake yote.

Alitangazwa na Papa Klementi V kuwa mtakatifu tarehe 5 Mei 1313[7].

Sikukuu yake ni tarehe 19 Mei[8].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Celestino V kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.