Papa Simplicio

(Elekezwa kutoka Papa Simplicius)

Papa Simplicio alikuwa Papa kuanzia tarehe 3 Machi 468 hadi kifo chake tarehe 10 Machi 483[1]. Alitokea Tivoli, Roma, Italia. Baba yake aliitwa Castinus[2] .

Mt. Simplisi.

Alimfuata Papa Hilarius akafuatwa na Papa Felix III.

Alitetea maamuzi ya Mtaguso wa Kalsedonia kwa kupinga uzushi wa Eutike[3][4] na alijitahidi kudhibiti matokeo ya uvamizi wa makabila ya Kigermanik walioteka Roma yenyewe na kumweka mfalme wa kwao, Odoakre, badala ya kaisari Romulus Augustus (476)[5] pamoja na kudumisha mamlaka ya Kanisa la Roma katika Ukristo wa Magharibi[2][6][7].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 10 Machi.[8]

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Vyanzo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Simplicio kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.