Stanislaus mfiadini

Stanislaus mfiadini (kwa Kipolandi:Stanisław Szczepanowski; 26 Julai 103011 Aprili 1079) alikuwa askofu wa Kraków[1] kuanzia mwaka 1072 hadi kifodini chake [2].

Mt. Stanislaus.

Kati ya maonevu ya wakati wake, alitetea kwa nguvu zake zote ustaarabu na tunu za Kikristo na kuongoza jimbo lake kama mchungaji mwema akisaidia maskini na kutembelea kila mwaka waklero wake.

Anajulikana hasa kwa kuuawa wakati wa kuadhimisha ibada na mfalme wa Polandi Bolesław II ambaye hakupenda makemeo yake makali.

Kwa sababu hiyo Stanislaus alitangazwa mtakatifu mfiadini na Papa Inosenti IV tarehe 17 Septemba 1253.

Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki kote duniani tarehe ya kifodini chake[3], lakini pia tarehe 7 Mei na 8 Mei, hasa nchini mwake.

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.