Theobadi wa Provins

Theobadi wa Provins, O.S.B. Cam. (kwa Kifaransa: Thibaud; 103330 Juni 1066) alikuwa mtoto wa mtawala wa Champagne, Ufaransa[1], aliyevutiwa sana na maisha ya Yohane Mbatizaji na ya Mababu wa jangwani[2], hivyo akaenda kujiunga na monasteri huko Reims.

Sanamu yake huko Joigny.

Baadaye, akiongozana na rafiki Walter, aliishi kama mkaapweke katika mahali na nchi mbalimbali ili kukwepa watu waliowatafuta ili kuwaheshimu[3].

Kabla hajafa alipewa upadrisho ili kuongoza vizuri zaidi wanafunzi alioanza kupokea akajiunga na Wabenedikto Wakamaldoli huko Sassano, Italia[4].

Papa Aleksanda II alimtangaza mtakatifu mwaka 1073.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Juni[5].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.