Muhammad Ali

Kwa watu wengine wenye jina hili tazama Muhammad Ali (maana)

Muhammad Ali

Takwimu
JinaMuhammad Ali
Jina la kuzaliwaCassius Marcellus Clay Jr.
Jina la utaniThe Greatest, The Champ,
The Louisville Lip
Urefu1.91 m (6 ft 3 in)
Kufikia2 M
Aina ya michezoMchezo wa ngumi
Mgawanyiko wa uzitoUzito mkubwa
UtaifaMarekani
Tarehe ya kuzaliwa17 Januari 1942 (1942-01-17) (umri 82)
Mahala pa kuzaliwaLouisville, Kentucky, U.S.
MsimamoOrthodox
Rekodi ya ndondi
Jumla ya mapigano61
Ameshinda56
Alizoshinda kwa kuangusha37
Alizopteza5
Sare0
Pambano asiloshiriki0

Muhammad Ali (jina la awali: Cassius Marcellus Clay Jr.; mnamo 17 Januari 1942 - 3 Juni 2016) alikuwa mwanamasumbwi kutoka nchini Marekani. Alipata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu. Katika mchezo wa ngumi anatazamwa kama mmoja wa wanamasumbwi bora wa uzito wa juu wa muda wote.

Wakati akiwa mwanamasumbwi wa ndondi za ridhaa, alishinda medali ya dhahabu ya uzito wa chini kwenye mashindano ya Olimpiki ya mwaka wa 1960 yaliyofanyika mjini Roma, Italia.

Baada ya kuwa mwanamasumbwi wa kulipwa, alikwenda kuwa mwanandondi wa kwanza kushinda mara tatu daraja la lineal. Mnamo mwaka wa 1999, Ali alipewa taji la "Mwanamichezo wa Karne" na Sports Illustrated na "Mwanamichezo Mashuhuri wa Karne" na BBC.[1]

Anafahamika sana kwa staili ya upiganaji wake, ambapo aliielezea staili yake kuwa ni "napaa kama kipepeo, nauma kama nyuki".[2]

Awali alijulikana kama Cassius Clay, lakini alibadilisha jina lake baada ya kujiunga na jumuia ya Kiislamu ya Nation of Islam mnamo mwaka wa 1964. Baadaye akabadilisha dini na kuwa Mwislamu kunako mwaka wa 1975.

Mnamo mwaka wa 1967, Ali alikataa kuwekwa katika orodha ya majeshi ya Marekani kutokana na imani ya kidini na kupinga vita dhidi ya Vietnam. Alikamatwa na kupatikana na hatia juu ya rasimu ya ukwepaji mashtaka, wakamvua taji lake la uanamasumbwi, na leseni yake ya uanamasumbwi ikazuiliwa. Hakufungwa, lakini hakupambana kwa takriban miaka minne mpaka hapo rufaa yake ilipofanyiwa kazi na Mahakama Kuu ya Marekani, ambapo akaja kushinda.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muhammad Ali kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.