Yared wa Ethiopia

(Elekezwa kutoka Yared)

Yared wa Ethiopia (kwa Kige'ez: ቅዱስ ያሬድ; 25 Aprili 505 - 20 Mei 571[1][2]) ni kati ya Wakristo maarufu wa Ethiopia[3].

Mt. Yared alivyochorwa karne ya 15.

Aliishi katika Ufalme wa Axum katika karne ya 6. Anatajwa kama mtunzi na mwanzilishi wa muziki wa Kikristo nchini, muziki wa utamaduni wa Ethiopia na wa Eritrea. Alikuza muziki wa kidini wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia, na matumizi katika muziki wa liturujia, pamoja na mfumo wa nota wa Ethiopia. Zaidi ya hayo, alitunga Zema, au mapokeo ya nyimbo za Ethiopia-Eritrea, ambazo zinaimbwa hadi leo.[4]

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Mei.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.