Zakaria (Injili)
Zakaria (kwa Kiebrania זכריה, Zekariah; kwa Kigiriki Ζαχαρίας, Zakarias; kwa Kiarabu زَكَرِيَّا, Zakariya; maana yake ni "YHWH amekumbuka") alikuwa kuhani mwaminifu wa Israeli katika karne ya 1 KK. Mke wake aliitwa Elizabeti, naye pia alikuwa wa ukoo wa Haruni.
Hawakupata mtoto hadi uzeeni kutokana na utasa wa mwanamke, lakini hatimaye walijaliwa kumzaa Yohane Mbatizaji.
Wote wanaheshimiwa kama watakatifu. Sikukuu ya wazazi ni tarehe 5 au 23 Septemba[1], kadiri ya madhehebu. Pengine wanaheshimiwa pamoja na mtoto wao tarehe 24 Juni.
Katika Injili
Habari hizo zinapatikana hasa katika Injili ya Luka, sura ya 1 na ya 2. Humo inaelezwa alivyopashwa na malaika Gabrieli kwamba atapata mtoto wa kiume ambaye atakakuwa nabii mkuu na kumtangulia Bwana[2].
Ingawa Zakaria hakusadiki mara, na kwa sababu hiyo aliadhibiwa kwa kufanywa bubu na kiziwi hadi ahadi itimie, siku ya kumtahiri mtoto alifungua tena kinywa chake na kutoa unabii.
Kadiri ya Lk 1:68-79, siku hiyo Zakaria alitunga wimbo ambao ni maarufu kwa jina la neno la kwanza katika tafsiri ya Kilatini, Benedictus (yaani "Asifiwe"). Katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, wimbo huo wa Kiinjili unatumika kila siku katika Masifu ya asubuhi.
Katika Kurani
Hata Kurani inamtaja mara kadhaa kama nabii na mzazi wa nabii Yahya, hasa katika sura ya 3 na ya 19.
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
- Prophet Zachariah the father of St John the Baptist Orthodox icon and synaxarion
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zakaria (Injili) kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |