Ziwa Maracaibo

Ziwa Maracaibo (Kihispania: Lago de Maracaibo) ni eneo kubwa la maji nchini Venezuela karibu na Bahari ya Atlantiki. Limeunganishwa na Bahari Karibi kwa njia ya mfereji wenye upana wa km 5.5. Kupitia mfereji huo maji ya chumvi hungia ndani yake. Kwa upande mwingine ziwa linalishwa na mito mingi. Upande wa kaskazini maji yake huwa ya chumvi-chumvi, upande wa kusini huwa maji matamu. Hivyo lina tabia ya hori ya bahari lakini pia ya ziwa [1] [2] [3] [4]. Kwa kawaida huitwa "ziwa", si "hori"[5].

Ziwa Maracaibo
Nchi zinazopakanaVenezuela
Eneo la majikm2 13,512
Kina cha chinim 60
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
m 0
Miji mikubwa ufukoniMaracaibo, Cabimas, Ciudad Ojeda

Jina lake limetokana na mji wa Maracaibo, ambao upo upande wa mashariki mwa mfereji wa kuingia baharini. Pale Maracaibo mfereji huwa na upana wa km 8.5 ukivukwa kwa daraja refu. [6]

Ziwa Maracaibo huwa na vipimo vya km 160 kwa km 110. Idadi ya mito inayoishia humo ni 135 na mkubwa kati yake ni Mto Catatumbo.

Umuhimu wa uchumi

Meli za baharini zinaweza kuingia ndani ya Ziwa Maracaibo na kupeleka mizigo kwenda bandari za Maracaibo na Cabimas.

Tangu mwaka 1914, mafuta ya petroli yamepatikana katika ziwa. Hadi leo ziwa na mazingira yake ni kitovu cha uzalishaji wa mafuta nchini Venezuela. [7] Takribani robo ya wakazi wa Venezuela wanaishi katika bonde karibu na ziwa. [8]

Shida za mazingira

Ekolojia ya ziwa huwa na matatizo, Miji mikubwa kando yake humwaga majitaka mle. Pia uzalishaji wa mafuta husababisha mara kwa mara machafuko.

Marejeo

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Maracaibo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.