Nenda kwa yaliyomo

Cesidio Giacomantonio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha halisi ya Mt. Cesidio wa Fossa kabla hajaondoka Italia kwenda China.

Cesidio Giacomantonio (Fossa, Italia, 30 Agosti 1873 - Hengzhou, 4 Julai 1900) alikuwa padri wa shirika la Ndugu Wadogo Wareformati aliyefia dini China alipokuwa mmisionari kwa kupigwa mawe na hatimaye kuchomwa moto akiwa hai ndani ya blanketi lililotiwa petroli alipokuwa anajaribu kuokoa Ekaristi wakati wa Uasi wa Waboksa[1].

Anaheshimiwa na Kanisa hilo kama mtakatifu mfiadini tangu tarehe 1 Oktoba 2000, alipotangazwa na Papa Yohane Paulo II pamoja na wenzake 119 maarufu kama wafiadini wa China.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila mwaka tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 4 Julai[2].

Tazama piahariri chanzo

Tanbihihariri chanzo

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoShairiJumuiya ya Afrika MasharikiUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaFasihi simuliziNembo ya TanzaniaMshororoMikoa ya TanzaniaVivumishiOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoPentekosteAina za manenoTanzaniaKamusi za KiswahiliMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaOrodha ya makabila ya TanzaniaAfrika Mashariki 1800-1845Orodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaUpendo Furaha PenezaMafurikoMisimu (lugha)KumaKisaweSentensiDiamond PlatnumzKamusi ya Kiswahili sanifuKamusiMisemoMaudhuiSimba S.C.Ukwapi na utaoTanganyikaOrodha ya Watakatifu WakristoNgeliLahaja za KiswahiliMaumivu ya kiunoRoho MtakatifuNomino