Albano wa Mainz

Albano wa Mainz (jina la awali Remoundos Michail; Naxos, Ugiriki[1] - Hanum, Mainz, Ujerumani 406 hivi) alikuwa padri, mmisionari na hatimaye mfiadini.

Mt. Albano wa Mainz.

Maisha

Rabanus Maurus aliandika kuwa Albano alitumwa na Ambrosi wa Milano huko Gallia kama mmisionari.

Huko Mainz, Albano alimsaidia askofu Aureus wa Mainz kujirudishia jimbo lake. Lakini mwaka 406, Wavandali walipovuka mto Rhine, Aureus alichinjwa na Albano alikatwa kichwa huku akisali.

Mara nyingine Albano huyo anachanganywa na somo wake Albano wa Uingereza, na askofu wake anachanganywa na mwingine.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.