Frank Zappa

Frank Vincent Zappa (21 Desemba 1940 - 4 Desemba 1993) alikuwa mwanamuziki na mtunzi kutoka nchini Marekani. Alijulikana kwa mtindo wake wa muziki, ambao mara nyingi ulikuwa wa ajabu na wa kuchekesha. Alitunga aina mbalimbali za muziki na albamu nyingi. Zappa alishirikiana na wanamuziki wengine wengi, haswa kundi lake la miaka ya mwongo wa 1960 The Mothers of Invention[1] na rafiki yake mwimbaji wa blues Captain Beefheart[2]. Watu wengine walimtaja kati ya watunzi bora katika muziki wa pop au hata muziki wowote usio wa classical[3][4].

Frank Zappa

Maisha

Zappa alizaliwa mjini Baltimore, Maryland na wazazi wahamiaji kutoka Italia, lakini alitumia muda mwingi wa maisha yake kusini mwa Kalifornia[5]. Alikulia Baltimore, Florida, na Monterey, Claremont na El Cajon, Kalifornia.

Zappa alizaa watoto wanne na mkewe Gail. Waliwapa wote majina yasiyo ya kawaida sana: Moon Unit, Dweezil, Ahmet, na Diva.

Zappa alipinga waziwazi madawa ya kulevya[6], mahubiri ya runinga, na namna zote za kudhibiti muziki.

Zappa alifariki dunia kutokana na saratani ya kibofu huko Los Angeles, Kalifornia.

Tovuti za nje

Tanbihi