Kipimo cha Beaufort

Kipimo cha Beaufort (ing. Beaufort scale) ni mfumo wa kupima kasi ya upepo. Msingi wake si kipimo kamili cha mwendo wa upepo bali kutazama matokeo ya upepo katika mazingira. Mfumo huu hutumiwa zaidi duniani ulianzshwa mnamo 1805 na MWingereza Francis Beaufort.

picha ya data inayoonyesha kiwango cha nguvu ya upepo wa Beaufort katika vitengo vya ukubwa, mafundo, na mita / sekunde.

Kuna ngazi 12 halafu ngazi ya "sifuri" kama hakuna upepo kabisa.

Ngazi za Beaufort

Namba ya BeaufortKasi ya upepoMaelezoKimo cha mawimbi bahariniDalili kwenye uso wa majiDalili kwenye nchi kavuPicha
km/hmphktsm/smft
0<1<1<1<0.3Kimya00tambarare.Kimya. Moshi hupanda bila kunyoka.
11-51-31-20.3-1.5Mwendo kidogo sana0.10.33Alama za mawimbi madogoMoshi inanyoka kidogo upande
26-113-73-61.5-3.3Upepezi mwepesi0.20.66Mawimbi madogo, vichwa kama kioo.Upepo husikika kwenye ngozi, majani yanatoa sauti
312-198-127-103.3-5.5Upepezi0.62Mawimbi, vichwa vinaanza kuwa vyeupe.Majani na matawi madogo yanaonyesha mwendo mfululizo
420-2813-1711-155.5-8.0Upepezi kiasi13.3Mawimbi madogoVumbi na na vipande vya karatasi vinasukumwa
529-3818-2416-208.0-10.8Upepo mwepesi26.6Mawimbi marefu kiasi (zaidi ya mita 1); pofu inaanza kuoekana juu ya mawimbiMatawi ya wastani huonyesha mwendo. Miti midogo huanza kuyugayuga.
639-4925-3021-2610.8-13.9Upepo39.9Mawimbi makubwa, vichwa vyeupe na pofu kila mahaliMatawi makubwa huonyesha mwendo. Mliohusikika kutoka nyaya za simu au umeme. Matumizi ya mwamvuli vigumu.
750-6131-3827-3313.9-17.2Upepo mkali413.1Mawimbi yanauja juu, pofu inaanza kuleaShina za miti huonyesha mwendo. Kutembea dhidi ya upepo kunahitaji nguvu.
862-7439-4634-4017.2-20.7Dhoruba mwepesi5.518Mawimbi marefu zaidi, huonyesha machafuko, povu nyingimatawi madogo yanavunjika. Ugumu wa kuendesha magari.
975-8847-5441-4720.7-24.5Dhoruba723Mawimbi marefu, kimo 6-7 m, povu nyingi sana. Vichwa vya mawimbi huvunjikaMatawi ya miti inavunjika, miti midogo inaanza kuanguka.
1089-10255-6348-5524.5-28.4Dhoruba kamili929.5Mawimbi marefu sana, bahari yote huonekana nyeupe. Kuona ni vigumu kutokana pofu nyingi hewaniMiti inavunjika, mabati yasiyofungwa vema yanapulizwa mbali, vipande vya lami visivyo imara vinasukumwa.
11103-11764-7256-6328.4-32.6Dhoruba kali11.537.7Mawimbi marefu mno, haiwezekani kuona mbaliUharibifu mwingi wa mimea. Paa za nyumba zinarushwa, vipande vikubwa vya lami iliyokatika pia
12≥118≥73≥64≥32.6Tufani≥14≥46Mawimbi vya kijituUharibifu wa mimea unazidi; madirisha huvunjika, majengo mepesi yanaharibika, magari yanaweza kusukumwa, hatari kutokana na takataka inayorushwa.

Picha

Other websites