Kupooza kwa ubongo

Kupooza kwa ubongo (KU) ki kikundi cha kudumu mwenendo wa ugonjwa inayotokea mapema katika maisha ya utotoni. Dalili na ishara zinatofautiana kwa watu. Kwa kawaida matatizo hujumuisha: uratibu duni, misuli ngumu, misuli dhaifu, tatizo la kumeza au kuzungumza, na mitetemekona mengine. Kunaweza pia kuwa na matatizo ya hisia, kuona, na kusikia. Kwa kawaida watoto wachanga walio na KU hawapinduki, hawaketi, hawatambai, au kutembea mapema kama ilivyo kwa watoto wengine wa umri wao. Ugumu wa uwezo wa kufikiria au kuwaza na kifafa kila moja hutokea kwa thuluti moja ya hali hiyo. Ilhali dalili zinaweza kuonekana kwa miaka michache ya kwanza ya maisha, matatizo yaliyoopo hayatazidi.[1]

Kupooza kwa ubongo
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyNeurology, pediatrics Edit this on Wikidata
ICD-10G80.
ICD-9343
OMIM603513 605388
DiseasesDB2232
MedlinePlus000716
eMedicineneuro/533 pmr/24
MeSHD002547

Kisababishi na utambuzi

Kupooza kwa ubongo husababishwa na ukuaji usiokuwa wa kawaida au kuharibika kwa sehemu za ubongo zinazodhibiti mwenendo, usawa, na hali ya mkao.[2][1] Kwa kawaida matatizo mengi hutokea wakati wa ujauzito; hata hivyo, yanaweza pia kutokea wakati wa kuzaliwa kwa mtoto, au muda mfupi baada ya kuzaliwa. Kawaida kisababishi hakijulikani. Vipengele vya hatari vinajumuisha kuzaliwa kabla ya wakati, kuwa pacha, maambukizi fulani wakati wa ujauzito kama vile toksoplasmosi au rubela, kuathiriwa na methylmercury wakati wa ujauzito, na jeraha la kichwa miaka ya kwanza ya maisha, na mengineyo.[1] takriban asilimia 2 ya kesi hizi zinaaminika kuwa kisababishi cha jenetiki kilichorithiwa.[3] Baadhi ya aina ya vikundi vinaainishwa kulingana na matatizo maalum yaliyoopo kwa sasa. Kwa mfano wale walio na misuli ngumu wana upoozaji wa ubongo wa ghafla, wale walio na uratibu duni wana upoozaji wa ubongo wa kuyumbayumba, na wale walio na matatizo ya kutembea wana upoozaji wa ubongo wa athetosisi. Utambuzi unategemea ukuaji wa mtoto kwa muda. Uchunguzi wa damu na picha ya matibabu inaweza kutumiwa kukomesha visababishi vingine.[1]

Uzuiaji na matibabu

KU unaweza kuzuiliwa kiasi kupitia kuchanja mama na juhudi za kuzuia majereha ya kichwa kwa watoto kama vile kupitia usalama ulioboreshwa. hakuna tiba kwa KU; hata hivyo, matibabu ya kudhibiti, matumizi ya dawa, na upasuaji inaweza kusaidia watu. Hii inaweza kujumuisha tiba ya kunyoosha viungo na tiba ya matatizo ya kuzungumza. Matumizi ya dawa kama vile diazepam, baklofeni, and botulinamu inaweza kusaidia kupumzisha misuli. Upasuaji unaweza kujumuisha kurefusha misuli na kukata iliyozidi neva. Kwa kawaida vifaa vya nje na teknolojia zingine za usaidizi ni za maana. Baadhi ya watoto wana maisha inayokabiribiana na ya watu wakubwa na matibabu bora. While dawa mbadalahutumika kila wakati hakuna ushahidi wa kusaidia matumizi yao.[1]

Epidemiolojia na historia

KU ni ugonjwa wa mwenendo ulio kawaida kwa watoto.[4] Hutokea kwa takriban 2.1 kwa uzazi 1000.[5] Kupooza kwa ubongo umeathiriwa binadamu tangu miaka ya kitambo. Maelezo ya kwanza ya hali hii imelezwa kwa kazi ya Hippocrates katika karne ya 5. Uchunguzi wa kina wa hali hii ulianza mnamo karne ya 19 na William John Little.[6] Baadhi ya uwezo wa matibabu zinachunguzwa, ikiwemo matibabu ya seli ya shina. Hata hivyo, uchunguzi zaidi unahitajika ili kubaini ikiwa ni salama na bora.[1]

Marejeo