Lea wa Roma

Lea wa Roma (alifariki Ostia, Roma, Italia, 384 hivi[1]) alikuwa mwanamke Mkristo wa mmojawapo kati ya koo maarufu zaidi za mji huo.

Mt. Lea.

Baada ya kufiwa mumewe alijitosa katika mambo ya dini na kuishi kitawa pamoja na Marsela wa Roma na wanawake wengine kadhaa kwa kuzingatia sala, malipizi na matendo ya huruma. Marsela alimkabidhi kazi ya kulea wasichana[2][3][4].

Jeromu aliandika sifa zake[5].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 22 Machi[6].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • Monks of Ramsgate.ea Book of Saints, 1921.. CatholicSaints.Info. 4 November 2014. Web. 12 January 2018.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.