Marsela wa Roma

Marsela wa Roma (Roma, Italia, 330 hivi - Roma, 410) alikuwa mwanamke Mkristo wa mmojawapo kati ya koo maarufu zaidi za mji huo.

Baada ya kufiwa mumewe alijitosa katika mambo ya dini na kuishi kama kitawa sawa na Paula wa Roma na wanawake wengine kadhaa kwa kuzingatia sala, malipizi na matendo ya huruma.

Jeromu aliandikiana naye[1] na kutunga kitabu[2] juu ya maisha yake akimsifu sana, kwamba kwa kukataa utajiri na umaarufu akastahili heshima zaidi kwa ufukara na unyenyekevu wake.[3].

Roma ilipotekwa na Waostrogothi, Marsela aliteswa akafa kutokana na majeraha aliyopata.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 31 Januari[4].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • Kraemer, Ross S., ed. Maenads, Martyrs, Matrons, Monastics: A Sourcebook on Women's Religions in the Greco-Roman World. 1988; rev. ed., Oxford and New York: Oxford University Press, 2004.
  • Wright, F. A., trans. Jerome: Select Letters. 1933; reprint ed., Cambridge, Mass.: Harvard University Press, 1999.

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.