Mkoa wa Kilimanjaro


Mkoa wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 25000.

Mkoa wa Kilimanjaro
Mahali paMkoa wa Kilimanjaro
Mahali paMkoa wa Kilimanjaro
Mahali pa Mkoa wa Kilimanjaro katika nchi ya Tanzania
Majiranukta: 3°20′S 37°20′E / 3.333°S 37.333°E / -3.333; 37.333
NchiTanzania
Wilaya7
Mji mkuuMoshi
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa
Eneo
 - Jumla13,209 km²
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 1,861,934
Tovuti:  http://www.kilimanjaro.go.tz/

Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kupita yote barani Afrika, umo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. Jina la mlima huu ndilo limeupatia mkoa jina lake.

Mkoa wa Kilimanjaro umepakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa kusini na mikoa ya Manyara na Arusha upande wa magharibi.

Wakazi

Mkoani Kilimanjaro kuna wakazi wapatao 1,861,934 (sensa ya mwaka 2022[1].).

Makabila makubwa mkoani humo ni Wachagga, Wagweno na Wapare, ambapo pia kuna makabila mengine madogomadogo kama Wamasai na Wakamba.

Makao makuu ya mkoa huu ni Moshi.

Katika sekta ya elimu wakazi wameendelea kidogo kwa maeneo ya mjini, lakini katika sehemu za vijijini elimu bado inatetereka kwa kiasi kikubwa, maana teknolojia ya utandawazi katika eneo kubwa haijashamiri.

Wilaya

Mkoa wa Kilimanjaro una wilaya 7 ambazo ni: Hai, Mwanga, Moshi mjini, Moshi vijijini, Rombo na Same na ile mpya ya Siha.

RamaniWilaya au manisipaaWakazi (2022)TarafaKataKijijiEneo km²
Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro
Wilaya ya Hai240,999171,217
Wilaya ya Moshi Vijijini535,803321,300
Wilaya ya Moshi Mjini331,7332163
Wilaya ya Mwanga148,763201,831
Wilaya ya Rombo275,314281,471
Wilaya ya Same300,303346,221
Wilaya ya Siha139,019171,217
Jumla1,861,93415213,209
Wilaya ya Siha hii ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Hai.
Marejeo: Mkoa wa Kilimanjaro

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

  • Hai
  • Siha
  • Moshi Mjini
  • Mwanga
  • Same Mashiriki
  • Same Magharibi
  • Moshi Vijijini
  • Vunjo
  • Rombo

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Kilimanjaro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.