Mkoa wa Mwanza

Mkoa wa Tanzania


Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, wenye postikodi namba 33000.

Mkoa wa Mwanza
Mahali paMkoa wa Mwanza
Mahali paMkoa wa Mwanza
Mahali pa Mkoa wa Mwanza katika Tanzania
Majiranukta: 2°45′S 32°45′E / 2.750°S 32.750°E / -2.750; 32.750
NchiTanzania
Wilaya8
Mji mkuuMwanza
Serikali
 - Mkuu wa MkoaAbas Kandoro
Eneo
 - Jumla19,592 km²
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 3,699,872
Tovuti:  http://www.mwanza.go.tz/
Mwanza

Umepakana na Geita upande wa magharibi, Shinyanga na Simiyu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.

Makao makuu ya mkoa yapo Mwanza mjini.

Mkoa una wakazi 3,699,872 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [1].

Kabla ya kumegwa na kuzaa mkoa mpya wa Geita, mkoa wa Mwanza ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2.

Wilaya

Wilaya ndizo Ukerewe, Magu, Sengerema, Buchosa, Misungwi, Kwimba, Nyamagana na Ilemela. Jiji la Mwanza ndani yake lina wilaya za Nyamagana na Ilemela.

Ramani (kabla ya 2012)Wilaya au manisipaaWakazi (2022)TarafaKataKijijiEneo km²
Wilaya za Mkoa wa Mwanza
Wilaya ya Buchosa413,110
Wilaya ya Ilemela509,687
Wilaya ya Kwimba480,025
Wilaya ya Magu421,119
Wilaya ya Misungwi467,867
Wilaya ya Nyamagana594,834
Wilaya ya Sengerema425,415
Wilaya ya Ukerewe387,815
Jumla3,699,872
Marejeo: Mkoa wa Mwanza

Wakazi

Makabila makubwa ya Mwanza ndio Wasukuma na Wazinza upande wa bara, halafu Wakerewe na Wakara visiwani.

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia

Mwamba wa Bismarck ziwani.

Tanbihi

Viungo vya nje


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Mwanza kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.