Mkoa wa Katavi


Mkoa wa Katavi ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 50000. Ulianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 kwa kumega mkoa wa Rukwa.

Mkoa wa Katavi
Mahali paMkoa wa Katavi
Mahali paMkoa wa Katavi
Location in Tanzania
NchiTanzania
KandaNyanda za Juu ua Kusini
Serikali
 - Mkuu wa MkoaRajab Mtumwa
Eneo
 - Jumla45,843 km²
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 1,152,958
EAT (UTC+3)
Msimbo wa posta50xxx
Kodi ya simu025
Tovuti:  katavi.go.tz

Makao makuu yako Mpanda.

Wilaya

Wilaya za mkoa huo ni tano tu: Mlele, Nsimbo, Mpanda mjini, Tanganyika (awali Mpanda vijijini) na wilaya ya Mpimbwe.

Wakazi

Katika sensa ya mwaka 2022 idadi ya wakazi ilihesabiwa kuwa 1,152,958 [1].

Utamaduni

Kabila kubwa ni lile la Wafipa; pia kuna Wabende, Wapimbwe na Wakonongo na dini yao kwa kiasi kikubwa sana ni Ukristo wa madhehebu ya Kanisa Katoliki.

Wapimbwe wanapatikana katika maeneo ya wilaya ya Mpimbwe katika vijiji vya Mamba, Mpimbwe na Majimoto. Katika kijiji cha Mamba kuna kivutio kizuri: bwawa kubwa la asili la maji ya moto ambayo hayapoi muda wote, ni ya moto iwe mchana au usiku.

Pia kuna sehemu za mkoa huu ni wa kihistoria katika baadhi ya maeneo. Mfano mtaa wa Madukani ambao walikua wakiishi Wahindi na Waarabu wa Oman kama Mzee Yusuf Al Salmi.

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

  • Katavi:mbunge ni Issack Kamwele(CCM)
  • Kavuu:mbunge ni Dk. Pudenciana Kikwembe(CCM)
  • Mpanda Mjini:mbunge ni Sebastian Kapufi(CCM)
  • Mpanda Vijijini:mbunge ni Moshi Selemani Kakoso(CCM)
  • Nsimbo:mbunge ni Richard Mbogo(CCM)

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Viungo vya nje


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Katavi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.