Jehanum

(Elekezwa kutoka Moto wa milele)

31°46′6.262″N 35°13′49.58″E / 31.76840611°N 35.2304389°E / 31.76840611; 35.2304389

Bonde la Hinnom, mwaka 1900 hivi.
Bonde hilohilo mwaka 2007.

Jehanum ni neno lenye asili ya Kiebrania (גיא בן הינום‎, Gei Ben-Hinnom, "bonde la mwana wa Hinnom"; kwa Kigiriki: γέεννα) linalomaanisha adhabu ya moto wa milele ambayo kadiri ya Biblia na Kurani itawapata watu waovu huko ahera kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu.

Kwanza Gehinnom (גהנום‎/גהנם‎) ni jina la bonde karibu na Yerusalemu lililotazamwa kama laaniwa (Yer 7:31, 19:2-6) kwa sababu ya maovu yaliyotendwa huko, hasa kuchinja watoto kwa heshima ya miungu.

Hata hivyo katika Agano Jipya jina hilo linatumika zaidi kwa maana ya moto wa milele[1], pia kwa sababu wakati wa Yesu bonde hilo lilitumika kama jalala, hivyo moto uliokuwa wa kudumu ndani yake. Katika Injili imeandikwa mara 11 kwamba mwenyewe alitumia jina hilo [2] kudokezea hali iliyo kinyume cha uzima wa milele[3].

Yesu alizungumzia moto wa milele, huku akitufunulia ukuu wa upendo wa Mungu, aliye heri yetu pekee. Alituangalisha juu ya hatari ya kutengana naye milele kwa dhambi. Mwenyewe atatoa hukumu hiyo: “Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake” (Math 25:41). “Humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki” (Mk 9:48). “Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku” (Ufu 14:11).

Katika Uislamu pia moto wa milele unaitwa جهنم, Jahannam[4]. Kurani inaitaja mara 77 kumbe haitaji kamwe kuzimu (هيدز).

Tanbihi

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.