Injili ya Marko
Injili ya Marko ni kitabu cha pili katika orodha ya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Huhesabiwa kati ya Injili Ndugu pamoja na Mathayo na Luka.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Yaliyomo yake ni habari za Yesu Kristo tangu kubatizwa kwake na Yohane Mbatizaji hadi ufufuko wake.
Mwandishi na wakati wa kuandikwa
Injili yenyewe haimtaji mwandishi wake.
Papias (mnamo mwaka 130) aliandika ya kwamba Yohane Marko alikuwa mwandishi wa taarifa hii. Huyu Yohane Marko anatajwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume kuwa mwenyeji wa Yerusalemu aliyemsindikiza Barnaba na Mtume Paulo kwenye safari yao ya kwanza. Papias alisema pia alikuwa mfasiri wa Mtume Petro aliyesikia jinsi Petro alivyosimulia habari za Yesu.
Baadhi ya wataalamu wa leo wana shaka juu ya huyu Marko kuwa mwandishi kwa sababu Injili yenyewe yaonyesha mwandishi wake hakujua vizuri sana habari za Uyahudi.
Kwa upande mwingine kuna pia mapokeo kuwa Marko huyu hakuwa mwenyeji wa Yerusalemu bali mtu mwenye asili ya Afrika ya Kaskazini aliyehamia Palestina baadaye.
Inaonekana ya kwamba Injili hiyo iliandikwa kabla ya maangamizi ya Yerusalemu mwaka 70 kwa sababu hakuna dalili ya kwamba mwandishi alikuwa na habari hii.
Inakubaliwa na wengi kwamba iliandikwa mjini Roma au walau nchini Italia baada tu ya dhuluma za Kaisari Nero dhidi ya Wakristo kuanza.
Yaliyomo
- Ufunguzi wa Injili (1:1-13)
- Yohane Mbatizaji (1:2-8)
- Ubatizo wa Yesu (1:9-11)
- Kujaribiwa kwa Yesu (1:12-13)
- Kazi ya Yesu katika Galilaya (1:14 - 9:50)
- Kazi ya Yesu katika Yudea na safari ya kwenda Yerusalemu (10)
- Kazi ya Yesu katika Yerusalemu na ziara ya Bethania (11 - 13)
- Kesi dhidi ya Yesu na mauti yake (14 - 15)
- Ufufuko wake (16)
Marejeo
Viungo vya nje
Tafsiri ya Kiswahili
- [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili.
Vitabu vingine
- A Brief Introduction to Mark Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Resources for the Book of Mark at The Text This Week
- An Online Textual Commentary on the Greek Gospels Archived 8 Juni 2008 at the Wayback Machine. by Wieland Willker, including detailed text-critical discussion of the 300 most important variants of the Greek text (PDF, 411 pages) and the variant endings (PDF, 17 pages).
- Catholic Commentary on Sacred Scripture Gospel of Mark, Author Dr. Mary Healy
Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Injili ya Marko kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |