Mtandao wa kijamii

Mtandao wa kijamii au Mitandao ya kijamii ni wavuti au huduma ambapo watu huongea, au hujumuishwa pamoja na watu wengine aidha ndani ya nchi au ulimwenguni kote.Huduma ya mitandao ya kijamii inaweza kuunganisha watu wenye shauku/mapenzi ya aina moja (kama vile mpira wa miguu, shule, ndondi, vyakula vya aina mbalimbali, filamu, dini na kadhalika) pamoja na urafiki.

Sehemu kubwa ya mitandao ya kijamii inakupa fursa ya kutengeneza taarifa zako katika ukurasa wako ikiwa ni pamoja na picha na maelezo kiasi kuhusu wewe mwenyewe, hasa yale ya msingi: unaishi wapi, una asili ya wapi, elimu, unapenda nini na kadhalika.

Mitandao ya kijamii ilianza kupendekeza tangu hatua za awali za uvumbuzi wa wavuti wa Walimwengu kwenye mwaka 1993.[1] Baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo ni maarufu sana ni pamoja na Facebook, Instagram, Twitter na JamiiTalk kwa Tanzania inasaidia kuongeza kasi ya mawasiliano ulimwenguni. Hata matumizi ya simu za mkononi zimeanza kupungua umaarufu wake hasa kwa mtindo wa uharaka wake wa kupeana jumbe kupitia mitandao hiyo.

Mitandao ya kijamii inatumika kuwaleta watu pamoja na kujenga urafiki miongoni mwao. Mitandao ya kijamii inatumika kupeana taarifa na watu wengine. Matumizi zaidi ya mitandao ya kijamii yanaendelea kuvumbuliwa katika nyanja tofauti ikiwemo elimu[2][3], biashara, matangazo ya kibiashara, siasa[4], ajira[5][6][7], afya na matibabu[8][9], utawala[10][11] na kadhalika.

Mitandao mingi ya kijamii inapatikana katika simu za mikononi hasa zile simujanja. Kuna baadhi ya makampuni yanafungia uwezo wa kuingia katika mitandao ya kijamii hasa kwa malalamiko ya kwamba waajiriwa wanapoteza muda mwingi katika mitandao hiyo.

Oroha ya mitandao ya kijamii

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.