Mwelekeo mkuu wa dira

Mwelekeo mkuu wa dira (kwa Kiingereza: cardinal direction au cardinal point) ni nukta nne zinazoonekana kwenye dira: Kaskazini, Mashariki, Kusini na Magharibi.

Dira inayoonyesha mielekeo mikuu.

Ufafanuzi wa mielekeo mikuu

Kaskazini na Kusini ni mielekeo ambayo hulenga ncha za kijiografia upande wa kusini na kaskazini wa Dunia. Mzunguko wa Dunia kwenye mhimili wake unafafanua Mashariki na Magharibi. Jua linachomoza kila asubuhi mashariki na kutua magharibi. Ncha za kijiografia za kaskazini na kusini ziko karibu na ncha sumaku za Dunia.

Kama sindano ina tabia ya sumaku na kuruhusiwa mwendo bila kuzuiwa (kwa mfano ikielea juu ya uso wa maji) itajipanga kulingana na uga sumaku wa Dunia kwa hiyo kujipanga kwa kuelekeza ncha zake kwenda ncha sumaku yaani kaskazini na kusini.

Kwenye dira sindano sumaku inaweza kucheza kwenye mhimili wake.

Tofauti baina ncha jiografia na ncha ya dira

Ilhali ncha sumaku kwa kawaida si sawa kamili na ncha za kijiografia kuna tofauti ndogo baina ya kaskazini ya dira na kaskazini ya kijiografia. Tofauti si muhimu sana katika maeneo yaliyo karibu na ikweta, huwa kubwa zaidi kadiri dira inavyotumiwa karibu zaidi na ncha za Dunia.

Mielekeo mikuu katika Kiswahili cha mabaharia

Kiswahili cha mabaharia kilikuwa na maneno mengine kama vile:

Tazama pia

Tanbihi