Papa Boniface I

Papa Boniface I alikuwa Papa kuanzia tarehe 28/29 Desemba 418 hadi kifo chake tarehe 4 Septemba 422[1]. Alitokea Roma, Italia, alipopewa ushemasi na Papa Damaso I.

Mt. Bonifas I.

Alimfuata Papa Zosimus[2] akafuatwa na Papa Selestino I.

Kabla ya kuchaguliwa Papa alikuwa balozi wa Papa Inosenti I huko Konstantinopoli[3].

Kama Papa alijitahidi kurudisha na kudumisha nidhamu ndani ya Kanisa[4] na kutetea mamlaka ya Kanisa la Roma katika Iliriko[5].

Alimuunga mkono Agostino wa Hippo dhidi ya uzushi wa Upelaji[6]

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 4 Septemba[7].

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Marejeo

  • Catholic Encyclopedia, Volume II. New York 1907, Robert Appleton Company. * Liber Pontificalis, toleo la Duchesne (Paris, 1886), 1, pp. lxii, 227-229;
  • Jaffe, Regesta Romanorum Pontificum (Leipzig, 1885), 1, 51-54;
  • Louis-Sébastien Le Nain de Tillemont, Mémoires (Venezia, 1732), XII, 385-407, 666-670;
  • Karl Joseph von Hefele, Conciliengeschichte and translation, §§ 120, 122;
  • Duchesne, Fastes Episcopaux de l'Ancienne Gaul (Paris, 1894), I 84-109;
  • Giovanni Sicari, «Reliquie Insigni e "Corpi Santi" a Roma», 1998.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Boniface I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.