Papa Leo II

Papa Leo II (jina la awali: Leo Maneius) alikuwa papa kuanzia Januari 681 au tarehe 17 Agosti 682 hadi kifo chake tarehe 3 Julai 683[1]. Alitokea kisiwa cha Sicilia, Italia[2][3] .

Mt. Leo II.

Jina la baba yake lilikuwa Paulo Manejo.

Alimfuata Papa Agatho, akafuatwa na Papa Benedikto II.

Waandishi wa wakati ule walimsifu kwa kuwa na elimu, kuhubiri vizuri na kutenda huruma kwa maskini na haki kwa wote[4].

Wakati wa Upapa wake alithibitisha Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli (680-681) uliofundisha rasmi kwamba Yesu, chini ya utashi wake wa Kimungu, alikuwa na utashi wa kibinadamu pia[5]. Pia alitangaza katika Kanisa la Magharibi maamuzi ya mtaguso mkuu huo ili yapokewe kote[6] na alimaliza kabisa farakano la Ravenna[7].

Mtaalamu wa Kigiriki na Kilatini[8], tena mpenzi wa muziki, alirekebisha ule wa Kigregori na kutunga tenzi mbalimbali kwa ajili ya Liturujia ya Vipindi.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe ya kifo chake[9].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Leo II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.