Paula wa Roma

Paula wa Roma (Roma, Italia, 5 Mei 347 - Bethlehemu, Israeli, 26 Januari 404[1]) alikuwa mwanamke Mkristo wa mmojawapo kati ya koo maarufu zaidi za mji huo[2].

Mt. Paula na masista wake walivyochorwa na André Reinoso katika karne ya 17, Lisbon, Ureno.

Aliolewa mapema akazaa watoto watano[3].

Alipokuwa na umri wa miaka 32 alifiwa mumewe akaendelea kutunza familia yake, lakini alizidi kuvutiwa na mambo ya dini na kuishi kama kitawa sawa na Marsela wa Roma na wanawake wengine kadhaa.

Mwaka 382 alikutana na Jeromu halafu akamfuata Bethlehemu katika monasteri zake (moja kwa wanaume na nyingine kwa wanawake[4][5] akamsaidia kutafsiri Biblia katika lugha ya Kilatini[6].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 26 Januari[7].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.