Rais wa Ujerumani

Rais wa Ujerumani ni mkuu wa dola katika Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.

Bendera ya Rais wa Ujerumani

Kazi yake ni kuwa alama ya umoja wa taifa, lakini katika mfumo wa serikali ya kibunge nchini Ujerumani hana madaraka mengi. Madaraka muhimu ya kisiasa ni kama yafuatayo

  • rais anapaswa kutia sahihi kwa kila sheria iliyopitishwa bungeni. Hapa anaweza kukataa akiona sababu muhimu ya kwamba sheria hailingani na katiba. Akikataa bunge ina njia ya kusahihisha sheria au kumshtaki ais mbele ya mahakama kuu. Tangu 1949 maraisi wa Ujerumani walikataa mara 9 kutia sahihi wakalazimisha serikali na bunge kubadilisha sheria.
  • rais anaamua kama bunge inavunjwa baada ya chansella kushindwa katika swali la imani katika serikali; chansella kama kiongozi wa serikali anaweza kudai kura ya bunge kama ina imani katika serikali. Kama swali hili linakataliwa na wabunge wengi chansella anaweza kumwomba rais kuvunja bunge na uchaguzi wa bunge jipya. Lakini azimio liko mkononi mwa rais anayeweza kumteua kiongozi wingine kuunda serikali mpya.

Rais huchaguliwa kila baada ya miaka 5 na mkutano wa shirikisho (Bundesversammlung) ambao ni wabunge wote pamoja na idadi sawa ya wawakilishi wa mabunge ya majimbo.

Mshahara wa rais ni asilimia 90 za mshahara wa chansella wa Ujerumani. Katika mwaka 2010 hii ililingana na Euro 199,000; pamoja na hayo anapata Euro 78.000 marupurupu ya kando na kwa pesa hii analipa mishahara ya watumishi wa nyumba yake anayopata bure.

Orodha ya marais wa Ujerumani

Marais wa Jamhuri ya Weimar (Reichspräsident) (1919-1933)

#PichaJina
(miaka ya maisha)
Tarehe ya kuanzaTarehe ya kwishaChama
1 Friedrich Ebert
(1871-1925)
11 Februari 191928 Februari 1925SPD
2 Paul von Hindenburg
(1847-1934)
12 Mei 19252 Agosti 1934-
Adolf Hitler
(1889-1945)
2 Agosti 193430 Aprili 1945NSDAP
3 Karl Dönitz
(1891-1980)
30 Aprili 194523 Mei 1945-

Marais wa Ujerumani ya Magharibi (1949–1990)

Marais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (Bundespräsident)

#PichaJina
(miaka ya maisha)
Tarehe ya kuanzaTarehe ya kwishaChama
1 Theodor Heuss
(1884-1963)
13 Septemba 194912 Septemba 1959FDP
2 Heinrich Lübke
(1894-1972)
13 Septemba 195930 Juni 1969CDU
3 Gustav Heinemann
(1899-1976)
1 Julai 196930 Juni 1974SPD
4 Walter Scheel
(born 1919)
1 Julai 197430 Juni 1979FDP
5 Karl Carstens
(1914-1992)
1 Julai 197930 Juni 1984CDU
6 Richard von Weizsäcker
(born 1920)
1 Julai 198430 Juni 1994CDU

Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (Präsident der Volkskammer)

#PichaJina
(miaka ya maisha)
Tarehe ya kuanzaTarehe ya kwishaChama
Wilhelm Pieck
(1876-1960)
11 Oktoba 19497 Septemba 1960SED
1 Walter Ulbricht
(1893-1973)
12 Septemba 19601 Agosti 1973SED
2 Willi Stoph
(1914-1999)
3 Oktoba 197329 Oktoba 1976SED
3 Erich Honecker
(1912-1994)
29 Oktoba 197618 Oktoba 1989SED
4 Egon Krenz
(1937-)
18 Oktoba 19896 Desemba 1989SED
5 Manfred Gerlach
(1928-)
6 Desemba 19895 Aprili 1990LDPD
Sabine Bergmann-Pohl
(1946-)
5 Aprili 19902 Oktoba 1990CDU

Marais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (Bundespräsident) (1990-sasa)

#PichaJina
(miaka ya maisha)
Tarehe ya kuanzaTarehe ya kwishaChama
6 Richard von Weizsäcker
(1920-)
since
1 Julai 1984
30 Juni 1994CDU
7 Roman Herzog
(1934-)
1 Julai 199430 Juni 1999CDU
8 Johannes Rau
(1931-2006)
1 Julai 199930 Juni 2004SPD
9 Horst Köhler
(1943-)
1 Julai 200431 Mei 2010CDU
10 Christian Wulff
(1959-)
2 Julai 201017 Februari 2012CDU
11 Joachim Gauck
(1940-)
18 Machi 2012sasa

Tazama pia