Tambarare ya Ulaya ya Mashariki

Tambarare ya Ulaya ya Mashariki inaenea katika Ulaya ya Mashariki, hasa katika Urusi. [1] Inaanza takribani kwenye longitudo ya nyuzi 26 ikielekea upande wa mashariki.

Tambarare hiyo inajumuisha mabeseni ya mito Dnepr, Oka, Don na Volga. Upande wa kusini mpaka uko kwenye safu za milima za Kaukazi na Krimea[2].

Upande wa magharibi inaendelea katika Tambarare ya Ulaya Kaskazini ilhali zote ni sehemu za Tambarare ya Ulaya (European Plain) katika Uholanzi, Ujerumani hadi kaskazini-mashariki mwa Poland). Ndiyo sehemu kubwa ya Ulaya isiyo na milima. [3]

Nyanda za Chini za Ulaya Mashariki. [4]

Nyanda za chini za Ulaya Mashariki zinajumuisha nchi za Kibalti, Belarusi, Ukraine, Moldova, Romania na sehemu ya Ulaya ya Urusi.

Eneo lote ni takriban kilometa mraba milioni 4 likiwa kwa wastani mita 170 juu ya UB.

Tanbihi

Marejeo

    • East European Plain at Ukrainian Soviet Encyclopedia
    • East European Plain at Great Soviet Encyclopedia

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tambarare ya Ulaya ya Mashariki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.