Theodori wa Tabennese

Theodori wa Tabennese (314 hivi - 27 Aprili 367) alikuwa mwandamizi wa kiroho wa Pakomi na alizuia shirikisho la kwanza la monasteri ya Kikristo lisiishe na kifo cha huyo mwanzilishi wake[1].

Picha takatifu ya Mt. Theodori wa Tabennese.

Zimebaki hotuba zake kadhaa katika maandishi ya wafuasi wake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa siku ya kifo chake[2] au tarehe 16 Mei, siku inayofuata sikukuu ya Pakomi[3].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.