Yohane Grande

Yohane Grande Román, O.H. (aliyependa kuitwa Yohane Mkosefu; Carmona, 6 Machi 1546 - Jerez de la Frontera, 3 Juni 1600) alikuwa bradha wa shirika la kihospitali la Mt. Yohane wa Mungu nchini Hispania.

Sanamu yake.

Kabla ya hapo alikuwa ameanzisha hospitali mwenyewe, ila aliamua kuiunga na shirika hilo mwaka 1574.

Aling'aa kwa upendo kwa wafungwa na waliotengwa na jamii: alipokuwa anahudumia wagonjwa wa tauni aliambukizwa akafa[1][2].

Papa Pius IX alimtangaza kwanza mwenye heri tarehe 13 Novemba 1858, halafu Yohane Paulo II akamtangaza mtakatifu tarehe 2 Juni 1992[3][4].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[5].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.