Zipu

Zipu ni kifaa kinachotumika kukutanisha upande mmoja na mwingine kwenye nguo, kitambaa, begi, midoli n.k. kama tunavyoona katika picha.

Zipu ikiunganisha pande mbili za kitambaa.

Historia

Zipu ilivumbuliwa na mhandisi Gideon Sundback aliyepata hataza mnamo mwaka 1909[1] na kuboreshwa naye hadi mwaka 1917.

Zipu zilianza kutumiwa kwa kufunga viatu na baada ya miaka kadhaa ziliingia katika soko la nguo.

Mwanzoni zilitengenezwa kwa metali lakini tangu miaka ya 1950 zipu za plastiki zimeenea.

Marejeo

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.