Nenda kwa yaliyomo

Sekunda wa Abitina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sekunda wa Abitina ni jina la wawili katika kundi la Wakristo 49 ambao mwaka 304, wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian, walihukumiwa kwa kuadhimisha Siku ya Bwana huko Abitinae[1][2][3], mji wa Afrika Kaskazini (leo Tunisia).

Tarehe 24 Februari mwaka 303, Diokletian alikuwa ametangaza hati yake ya kwanza dhidi ya Wakristo, akiagiza uteketezaji wa Biblia na maabadi ya Kikristo katika Dola la Roma lote, pamoja na kukataza Wakristo wasikutane kwa ajili ya ibada.[4]

Ingawa Fundanus, askofu wa Abitinae, alikubali kukabidhi maandiko matakatifu ya Kanisa kwa serikali, baadhi ya waamini waliendelea kukutana kwa siri chini ya padri Saturninus. Basi, walikamatwa na kupelekwa na mahakimu wa huko hadi Karthago, makao makuu ya mkoa, kwa ajili ya hukumu.[5]

Tarehe 12 Februari gavana Anullinus alisikiliza kesi. Mmoja wa watuhumiwa, Dativus, alikuwa mjumbe wa senati. Ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhojiwa, kuteswa na hatimaye kufa.[6][7]

Saturninus alifuata na kushika msimamo katika kuteswa. Wote walifanya vilevile, wanaume kwa wanawake wakiwemo watoto wake 4.

Kati ya majibu waliyotoa hao wafiadini, moja limetajwa mara nyingi: Emeritus, aliyekuwa mwenyeji wa wenzake, alipoulizwa kwa nini aliwakaribishwa kwa ibada kinyume cha sheria, alijibu: "Sine dominico non possumus" ("Hatuwezi kuisi bila ya Bwana").

Tangu kale wafiadini hao wote wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Februari. [8]

Orodha ya wafiadini wa Abitinahariri chanzo

Tazama piahariri chanzo

Tanbihihariri chanzo

Viungo vya njehariri chanzo

🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoFasihi simuliziAina za manenoShairiVivumishiMikoa ya TanzaniaOrodha ya makabila ya TanzaniaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaLughaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoKamusi za KiswahiliMofimuFasihiNembo ya TanzaniaMawasilianoSentensiMarie AntoinetteKamusiMange KimambiKumaViwakilishiAlama ya uakifishajiKitenziFani (fasihi)TamthiliaVitendawiliNominoKiswahiliMaudhuiSilabiTanzaniaJumuiya ya Afrika MasharikiKisaweVieleziYoung Africans S.C.Kiwakilishi nafsiDiamond Platnumz