Ana Schaeffer

Ana Schaeffer (Mindelstetten, Bavaria, Ujerumani, 18 Februari 1882 – Mindelstetten, 5 Oktoba 1925), alikuwa mwanamke mwenye karama za pekee katika maisha ya ugonjwa[1] nyumbani akizama katika sala.

Picha halisi ya Mt. Ana.

Mwaka 1910 alijikuta ana madonda mwilini kama yale ya Yesu msulubiwa[2]. Pia alipata njozi[3].

Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 7 Machi 1999[4], halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 21 Oktoba 2012[5].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Oktoba[6].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.