Cathay Pacific

Cathay Pacific Limited ni kampuni kuu ya ndege ya Hong Kong, China, ikiwa na makao yake makuu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ya Hong Kong.

Mnamo 2008, Cathay Pacific na Dragonair ilihudumu ndege 138,000, na kubeba wasafiriwa takriban milioni 25 na kubeba mizigo ya zaidi ya tani milioni 1.6.

Ndege hii ilianzishwa mnamo 24 Septemba 1946 na Mwamerika R|oy Farrell pamoja na Sydney de Kantzow anayetoka nchini Australia. Waliita Cathay Pacific kwa sababu Cathay ni jina la jadi la China; na Pacific kwa ajili Farey alikuwa na matumaini ya kuwa siku moja wataruka juu ya bahari ya Pacific.

Ndege aina ya Boeing 747-400 ikisafishwa kwenye unwnja wa ndege wa London Heathrow

Miji inayosafiria

Afrika

Asia

Asia Mashariki

ndege aina ya Boeing 777-200 mjini Nagoya, Japan
Cathay Pacific kwenye uwanja wa ndege wa Hong Kong International Airport

Asia Kusini

Uropa

Amerika ya Kaskazini

Oceania

Huduma

Chakula

chakula ndani ya Cathay Pacific First Class

Vyakula na vinywaji vinavyotolewa kwenye ndege zote zitokazo Hong Kong hutolewa na kampuni ya Cathay Pacific Catering Services.[1]

Huduma za ziada

Ndani ya ndege ya Cathay Pacific, kuna runinga kwenye kila kiti inayoonyesha sinema, filamu na muziki za Marekani na za Kihindi. Pia, kuna jalada na magazeti ya kusoma. Kila msafiri ana takriban filamu 100, vipindi 350, na albamu za muziki 880 na stesheni 22 za redio.

First Class

Cathay Pacific New First Class kwenye ndege ya aina Boeing 747-400

Viti vya First Class vinaweza kulazwa kama vitanda vya urefu wa inchi 36 x inchi 81. Viti hivi vina chombo cha kukandia mwili, kabati yenye vitu vya kibinafsi, na rununga ya inchi 17.

Business Class

New Business Class kwenye ndege ya Boeing 747-400

Viti hivi vya Business Class vimepangwa sawiya na vya Air Newzealand, Virgin Atlantic na Jet Airways. Viti vyake vinaweza kulazwa chini kama kitanda. Pia kuna chombo cha kukanda, na simu.[2]

Economy Class

Hapa, viti huweza kulazwa kidogo tu bila ya kumsumbua msafiri aliye nyuma. Kuna runinga yenye stesheni 25. Kila kiti ina mto wa kulalia.

Tuzo

Marejeo