Eulogi wa Aleksandria

Eulogi wa Aleksandria (kwa Kigiriki: Εὐλόγιος I; alifariki 13 Septemba 608) alikuwa Patriarki wa Kigiriki wa Aleksandria (Misri) tangu mwaka 580 hadi 608.

Mchoro mdogo katika Menologion of Basil II

Mwenye asili ya Syria, aliishi huko kama mmonaki padri.

Baada ya kuchaguliwa kuwa Patriarki, kwa elimu yake kubwa alipinga mafundisho ya Wamonofisiti na wengineo[1] akiungana na Papa Gregori I wa Roma [2] ambaye alimuandikia barua nyingi, akisema, "Si mbali nami aliye kitu kimoja nami" [3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake au 13 Februari au 13 Juni[4][5].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.