Gabrieli Lalemant

Gabrieli Lalemant, S.J. (Paris, Ufaransa 3 Oktoba 1610 – Waubaushene, karibu na Tay, Ontario, Kanada, 17 Machi 1649) alikuwa padri wa Wajesuiti mmisionari mwenye bidii ya ajabu kwa Wahuroni wa Amerika Kaskazini tangu mwaka 1646, aliyewatangazia utukufu wa Mungu kwa lugha yao[1].

Mt. Gabrieli alivyochorwa.
Wajesuiti wafiadini wa Amerika Kaskazini.

Alikamatwa pamoja na Waindio hao[2], akateswa sana akauawa na Wairoki, kabila lingine la Waindio.

Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 21 Juni 1925, na kuwa mtakatifu tarehe 29 Juni 1930[3].

Sikukuu ya kundi lake la wafiadini huadhimishwa tarehe 19 Oktoba, lakini ya kwake mwenyewe huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[4].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.