Janet Mbugua

Mwigizaji wa Afrika Kusini

Janet Mbugua - Ndichu (alizaliwa 10 Januari 1984) ni mwanahabari, mtangazaji na mwigizaji wa Kenya. Anajulikana kuwa alifanya kazi KTN apo mwanzo. Alifanya kazi kwenye chaneli ya Citizen TV kwa miaka kadhaa, kabla ya kutangaza kustaafu kwake kutoka kwenye tasnia hiyo ya habari. Alikuwa mtangazaji mkuu wa habari kwenye chaneli hiyo ya Citizen wakati wote, pamoja na Hussein Mohammed. Aliechukua nafasi kwenye Jumuiya ya Kibinadamu ya Msalaba Mwekundu ya Kenya. Janet anavutiwa na filamu na sanaa, kama mwigizaji aliyeongoza katika safu ya runinga ya Rush.

Janet Mbugua

Maisha ya awali na elimu

Janet alizaliwa na kukulia Mombasa, Kenya. Ana kaka pacha Timothy Mbugua.[1]

Janet alikwenda Shule ya sekondari ya Brookhouse na baadaye akajiunga na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani (USIU).

Baada ya kufanya kazi kwa muda, alijiunga na Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Ubunifu cha Limkokwing nchini Malaysia kwa shahada yake ya mawasiliano ya watu wengi.Alisomea MBA yake katika Global Business Management katika Swiss Management Academy mjini Nairobi, Kenya.

Kazi

Mnamo 2004, akiwa na umri wa miaka 19, Mbugua alianza kazi yake katika 98.4 Capital FM.[2]Mnamo 2009, aliajiriwa kama mtangazaji wa habari, ripota na mtayarishaji wa kipindi cha mambo ya sasa cha Pan-Afrikani, Afrika 360,[3] na e.tv huko Johannesburg, Afrika ya Kusini. Hadi hivi majuzi alikuwa mtangazaji wa habari katika runinga ya Citizen inayotangaza Jumatatu Maalumu na The Big Question.[4]

Mnamo 2014, aliigiza katika sitcom, Rush.[5] Aliigiza katika nafasi ya uongozi kama Pendo Adama,[6] mmiliki na mhariri mkuu wa Rush Magazine.[7]

Mnamo Julai 2017, alianza kushauriana na The Hive, Shirika la Marekani linalotaka kuongeza ujumbe wa Usawa wa Jinsia nchini Kenya na nchi nyingine za Afrika.[8] Mnamo 2019, alisimamia na kuandaa Kipindi cha Televisheni kilichopewa jina la Hapa na Sasa kwenye NTV(Here And Now on NTV), ambacho kiliangazia maswala ya kijamii na kiuchumi yanayoathiri vijana.[9][10]

Kazi za kibinadamu

Yeye ndiye mwanzilishi na mkurugenzi wa Media Avenue Limited, ambapo watu hupewa huduma kama vile kuzungumza kwa umma, kudhibiti na kuanza. Pia ameimarisha katika kuwawezesha vijana wa kike na kampeni ya Inua Dada[11] ambayo imeidhinishwa na mke wa rais wa Kenya, Margaret Kenyatta.[12]Mnamo tarehe 8 Oktoba 2021 alizindua Kituo cha Inua Dada katika makazi duni ya Korogocho jijini Nairobi . Kituo hiki ni sehemu inayotoa fursa ya kupata taarifa na ufahamu kuhusu afya ya uzazi na haki..

Maisha binafsi

Janet Mbugua ameolewa na Edward Ndichu.[13] Kwa pamoja wana watoto wawili wa kiume, Ethan Huru Ndichu aliyezaliwa Oktoba 2015 na Mali Ndichu.[14][15] Mnamo 2019, Janet alitoa kitabu chake cha kwanza, 'Wakati Wangu wa Kwanza', mkusanyiko wa hadithi fupi kutoka kwa wanawake, wasichana na wanaume juu ya mwingiliano wao wa kwanza na hedhi.[16][17]

Filamu zake

  • Rush  – Pendo Adama

Marejeo