Kopenhagen

Kopenhagen, Denmark


Mahali pa Kopenhagen katika Denmark

Eneo
 - Mji
 - Mkoa wa Jiji

88 km²
455.61 km²
Wakazi
(2006-01-01)
 - Mji
 - Mkoa wa Jiji
 - Msongamano (mji/jiji)


501,158
1,115,035
5695/km² / 2447/km²
Kanda la wakatiUlaya ya Kati: UTC+1
Latitudo
Longitudo
55°43' N
12°34' E

Kopenhagen (kwa Kidenmark: København = "Bandari ya wafanya biashara") ni mji mkuu wa Denmark pia mji mkubwa wa nchi na kitovu cha utawala, uchumi na utamaduni.

Sanamu ya Nguva Mdogo kufuatana na hadithi ya mshairi Mdani Hans Christian Andersen
Kopenhagen, picha ya angani
Katika mji wa kale ya Kopenhagen

Jiografia

Kopenhagen iko Zealand (Sjælland) ambacho ni kisiwa kikubwa cha Denmark. Iko karibu na mji wa Malmo katika Uswidi ulio ng'ambo ya mlango wa bahari ya Oresund unaounganisha bahari ya Baltiki na Kattegat kuelekea Bahari ya Kaskazini. Sehemu ndogo ya mji iko kwenye kisiwa cha Amager.

Eneo la Kopenhagen lina miji ya Kopenhagen yenyewe (wakazi 501,158), Frederiksberg (wakazi 91,855), Gentoftev (wakazi 68,623) na wakazi wengine 453,399 katika miji midogomidogo ndani ya wilaya ya Kopenhagen.

Mahali pa Kopenhagen panapopendekezwa

  • Palais Amalienborg
  • Bakken
  • Christiania
  • Christiansborg
  • Copenhagen Zoo
  • Makumbusho ya Sanaa ya Denmark
  • Bustani ya Wanyama
  • Kanisa la Mt. Alban
  • Jumba la Frederiksborg
  • Jumba la Kronborg
  • Nguva Mdogo
  • Makumbusho wa kitaifa
  • Bustani ya Tivoli
  • Opera ya Kopenhagen

Watu mashuhuri wenye uhusiano na Kopenhagen

  • Hans Christian Andersen - mshairi (karne ya 19)
  • Arne Jacobsen - msanifu majengo (karne ya 20)
  • Niels Bohr - mwanafizikia na mshindi wa tuzo ya Nobel (karne ya 20)
  • Tycho Brahe - mwanafalaki (karne ya 16)
  • Nicolai Grundtvig - mchungaji, mwanatheologia, mwalimu (karne ya 19)
  • Søren Kierkegaard - mwanafalsafa na mwanatheologia (karne ya 19)

Viungo vya Nje

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kopenhagen kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.