Maurice Jarre

Maurice-Alexis Jarre (13 Septemba 192428 Machi 2009)[1][2][3][4] alikuwa mtunzi wa vibwagizo vya filamu na mwongozaji muziki wa vyombo vingi kutoka nchini Ufaransa.

Japokuwa ametunga tungo kadhaa kwa ajili ya kazi za maonyesho ya muziki, alifahamika sana kwa utunzi wake wa vibwagizo vya filamu, na hasa kwa kufanya kazi pamoja na mwongozaji David Lean. Jarre ametarishaji vibwagizo karibuni vya filamu zote za Lean tangu Lawrence of Arabia (1962). Vibwagizo vingine maarufu ni pamoja na The Message (1976), Dead Poets Society (1989) na Ghost (1990). Jarre alizawadiwa nyota katika Hollywood Walk of Fame.[5]

Marejeo

Viungo vya Nje