Mpito wa Utaridi

Mpito wa Utaridi mbele ya Jua (kwa Kiingereza transit of Mercury) unatokea wakati sayari Utaridi (Mercury) inapita katika mstari baina ya jua na dunia.

Mpito wa Utaridi mnamo Novemba 11, 2019

Hii inalingana na kupatwa kwa jua kiasi. Ilihali Utaridi iko mbali inaonekana ndogo na kufunika sehemu ndogo ya jua tu kwa mtazamaji duniani.

Sayari ya Utaridi wakati huu inaonekana kama duara dogo jeusi linalopita polepole kwenye jua. Kwa kawaida mpito mmoja hudumu saa kadhaa.

Tazama pia

Marejeo


Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu: