Oscar Romero

Óscar Arnulfo Romero y Galdámez (15 Agosti 1917[1]24 Machi 1980[2][3][4]) alikuwa askofu mkuu wa Kanisa Katoliki huko San Salvador, nchini El Salvador kuanzia tarehe 21 Juni 1970 hadi kifodini chake[5].

Óscar Romero alivyochorwa na J. Puig Reixach (2013).
Ibada ya kumtangaza mwenye heri tarehe 23 Mei 2015 huko San Salvador.

Alipinga serikali kuhusu ufukara wa umati, dhuluma, mauaji na unyanyasaji katika jamii[6].

Baada ya vitisho mbalimbali, Romero aliuawa wakati anapoadhimisha Misa. Ingawa hakuna aliyehukumiwa kwa kumuua, kamati ya Umoja wa Mataifa imethibitisha kwamba aliuawa kwa agizo la mwanasiasa wa mrengo wa kulia Roberto D'Aubuisson[7][8]. Hatimaye mnamo Oktoba 2018 mahakama imeagiza mhusika mmojawapo akamatwe ingawa haijulikani yuko wapi, isipokuwa kwamba ameshahama El Salvador.

Kwa heshima yake, mwaka 2010, Mkutano Mkuu wa UM ulitangaza tarehe 24 Machi kuwa "Siku ya Kimataifa ya Haki za Kujua Ukweli kuhusu Uvunjaji wa Haki za Binadamu na ya Hadhi ya Wahanga" (International Day for the Right to the Truth Concerning Gross Human Rights Violations and for the Dignity of Victims)[9].

Papa Fransisko alimtangaza mwenye heri tarehe 23 Mei 2015[10] na mtakatifu tarehe 14 Oktoba 2018.

Anaheshimiwa na Wakristo kadhaa wa madhehebu mengine[11] pia kama mfiadini[12].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[13].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.