Papa Celestino I

(Elekezwa kutoka Papa Celestine I)

Papa Celestino I alikuwa Papa kuanzia tarehe 10 Septemba 422 hadi kifo chake tarehe 24 Julai 432[1]. Alitokea Campania, Italia na baba yake aliitwa Priscus.

Mtakatifu Selestino I.

Alimfuata Papa Boniface I akafuatwa na Papa Sixtus III.

Akiwa na juhudi za kulinda na kupanua Kanisa, alianzisha uaskofu katika visiwa vya Britania akaunga mkono Mtaguso wa Efeso katika kumuita Bikira Maria "Mama wa Mungu" dhidi ya mafundisho ya Nestori[2].

Alipambana pia na uzushi wa Upelaji [3] na kupigania nidhamu[4][5] pamoja na kudhibiti farakano la Novatianus[6].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 27 Julai[7] lakini pia 6 Aprili au 8 Aprili.

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Celestino I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.