Papa Telesphorus

(Elekezwa kutoka Papa Telesfori)

Papa Telesphorus alikuwa Papa kuanzia takriban 127/128 hadi kifo chake takriban 137/138[1]. Alikuwa na asili ya Ugiriki[2][3].

Papa Telesphorus

Alimfuata Papa Sixtus I akafuatwa na Papa Hyginus.

Alishughulikia liturujia ya Kanisa la Roma[4] bila kulazimisha majimbo mengine hata katika suala la Pasaka ya Kikristo lililoanza kujitokeza[5]. Kinyume chake, alipambana na uzushi wa Gnosi uliozidi kuenea jijini[6].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini[7].

Sikukuu yake ni tarehe 2 Januari[8].

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Marejeo

  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.
  • Kelly, J.N.D. Oxford Dictionary of Popes. (1986). Oxford, England: Oxford University Press.
  • Benedict XVI. The Roman Martyrology. Gardners Books, 2007. ISBN 978-0-548-13374-3.
  • Chapman, John. Studies on the Early Papacy. Port Washington, NY: Kennikat Press, 1971. ISBN 978-0-8046-1139-8.
  • Fortescue, Adrian, and Scott M. P. Reid. The Early Papacy: To the Synod of Chalcedon in 451. Southampton: Saint Austin Press, 1997. ISBN 978-1-901157-60-4.
  • Loomis, Louise Ropes. The Book of Popes (Liber Pontificalis). Merchantville, NJ: Evolution Publishing. ISBN 1-889758-86-8

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: